GET /api/v0.1/hansard/entries/1252754/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1252754,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1252754/?format=api",
"text_counter": 162,
"type": "speech",
"speaker_name": "Nyali, UDA",
"speaker_title": "Hon. Mohamed Ali",
"speaker": null,
"content": " Ahsante sana, Mhe. Spika. Ninasimama kuunga mkono. Vile vile, nitaanza kwa kusema kwamba ni vyema sisi, kama Wabunge, tujadili maswala muhimu katika taifa hili na wananchi wake. Ikiwa tutaanza kufanya mazungumzo ya kuleta uvumi na fitina, basi hatutakuwa tunasaidia mwananchi wa kawaida. Hili Bunge lina Wabunge wengi – zaidi ya 300 – na asilimia kubwa ni ya wale walio nje. Hawa Wabunge wakifika katika majukwaa, wanaenda kuchochea wananchi pasi na kuwaambia ukweli. Kuna Mbunge mmoja kutoka upande huu wetu ambaye pia ameenda kuchochea wananchi. Lakini leo hayuko katika Bunge hili kujadili maswala haya ya fedha ili kuwafanya Wakenya waelewe zaidi. Taifa hili limekuwa la omba omba tangu Kenya kupata Uhuru katika mwaka wa 1963. Kenya imekuwa ikiongozwa na maswala ya kukopa. Kila mwaka ni kukopa ili kulipa wafanyikazi wa Serikali, na kukopa ili kuleta maendeleo. Ndio maana imefika mahali ambapo tunasema kwamba tutajinyima na kujizuia dhidi ya mikopo ili tuanze kujifunza kutafuta hela miongoni mwa Wakenya na kujikomboa kutoka kwa minyororo ya kukopa kila mwaka. Taifa hili haliwezi kukopa hadi kiyama. Ni lazima taifa hili tukaze minyororo, tufunge long’i zetu vizuri, tuvae njuga, na tuhakikishe tutafanya hivi kwa mwaka mmoja au miwili hivi, halafu The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor."
}