GET /api/v0.1/hansard/entries/1252755/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1252755,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1252755/?format=api",
"text_counter": 163,
"type": "speech",
"speaker_name": "Nyali, UDA",
"speaker_title": "Hon. Mohamed Ali",
"speaker": null,
"content": "mambo yatakuwa sawa huko mbeleni. Unataka tujenge barabara wanazotaka wananchi vipi katika Kenya hii? Unataka tuunganishe umeme vipi? Unataka tupunguze bei ya vyakula vipi, ilihali tutaendelea kukopa kwa Wazungu ili kuleta matatizo kwa Afrika? Ni lazima tujifunze na kustahimili. Leo hii, Wabunge wenzangu katika Bunge hili wana nguvu kwa sababu kila Mbunge, kama sijakosea, ana nyumba. Wacha nizungumzie hili swala la nyumba, kwa sababu linachukuliwa vibaya sana. Mbunge wa Kenya anachukua Ksh30 milioni za kununua nyumba anapoingia Bungeni kila muhula. Hawa Wabunge wote, pia mimi, ninachukua hiyo pesa na kuhakikisha nimenunua nyumba."
}