GET /api/v0.1/hansard/entries/1252757/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1252757,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1252757/?format=api",
    "text_counter": 165,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Nyali, UDA",
    "speaker_title": "Hon. Mohamed Ali",
    "speaker": null,
    "content": "Mhe. Spika, nilinde dhidi ya maneno wanayoyasema. Wabunge, tuwache ubinafsi ili, kwa mara ya kwanza, tuwafikirie hawa wananchi. Ni lazima tujinyime na tujiadhibu ili tuwakomboe Wakenya. Leo unataka kupinga Mswada huu kwa sababu ya kutafuta umaarufu. Hizo ni siasa za populism. Tunataka siasa za kukomboa taifa hili. Hatuwezi kuwanyima maskini nyumba, ilhali wewe unajipatia nyumba kila mwaka."
}