GET /api/v0.1/hansard/entries/1252763/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1252763,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1252763/?format=api",
"text_counter": 171,
"type": "speech",
"speaker_name": "Nyali, UDA",
"speaker_title": "Hon. Mohamed Ali",
"speaker": null,
"content": "Angalia Mswada huu. Kwanza, unatupatia uhuru wa kuwapatia nafasi wawekezaji waje katika taifa hili. Wawekezaji wengi wataweza kuwekeza katika mji wa Nairobi kwa kuwa wamepunguziwa ushuru kutoka asilimia 37.5 hadi 30. Hii ni kwa masharti kwamba waende wawekeze katika maeneo mengine - Bungoma, Mombasa na Garissa, na sehemu ambazo hazina uwekezaji. Sehemu ambazo hazina uwekezaji zikiekezwa, basi watoto wetu watapata kazi na nchi itapata ushuru na nguvu za kujikomboa. Angalieni yaliyo mazuri ndani ya Mswada wa Fedha. Kwa mfano, asilimia kumi ambayo inalinda soko la ndani kwa kuhakikisha tunaenda kwa sekta ya juakali, tunanunua bidhaa za Kenya ili kuhakikisha tunainua viwanda vyetu. Angalieni yale mazuri; msiangalie ubinafsi, msiwe na tamaa, na msiongozwe na viongozi ambao hawana dira ya uongozi. Kila mwaka ni kusumbua; kila mwaka ni kuambia…"
}