GET /api/v0.1/hansard/entries/1252847/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1252847,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1252847/?format=api",
"text_counter": 255,
"type": "speech",
"speaker_name": "Kaloleni, ODM",
"speaker_title": "Hon. Paul Katana",
"speaker": null,
"content": " Asante, Mhe. Spika, kwa kunipa muda huu kuchangia Mswada huu wa Fedha wa 2023. Ninapinga Mswada huu kwa sababu gharama ya maisha imepanda kiwango kikubwa zaidi. Na gharama hii haijui ni nani yuko Upinzani na aliye ndani ya Serikali. Taabu hizi tunazipata sote kama Wakenya. Ukiangalia ile nyongeza ambayo inaongezwa kwa mafuta, ukiongeza ushuru kwa mafuta, utapata kila kitu kinapanda. Anayeumia zaidi ni yule ambaye alikuwa akiongelewa: mama mboga na waendeshaji wa bodaboda. Hii ni kwa sababu hakuna tofauti ya mama mboga, mwendeshaji bodaboda na Mbunge au Rais. Kama ni mafuta, tunanunua lita moja kwa bei sawia."
}