GET /api/v0.1/hansard/entries/1252848/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1252848,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1252848/?format=api",
    "text_counter": 256,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Kaloleni, ODM",
    "speaker_title": "Hon. Paul Katana",
    "speaker": null,
    "content": "Bw. Spika, wakati Serikali hii iliingia uongozini, iliahidi Wakenya kuwa gharama ya unga na ile ya bidhaa muhimu ingeshuka. Lakini kufikia sasa, gharama ya maisha imepanda maradufu. Kikwetu, tunajua dalili za mwanaume kuwa na mbegu za kuzalisha na kama hana utajua. Pale nyumbani, babako akiona mkaza mwana ameanza kutema tema mate, anajua ni dalili kwamba kumefanyika jambo na anatarajia mjukuu. Lakini, hatuoni dalili za kutema mate kutoka kwa Serikali hii. Kila siku wanatangaza tu kuwa, “Bibi yangu ana mimba” ila hatuioni. Tunahadaiwa. Serikali ilisema itashukisha gharama ya maisha. Wananchi wamesema tusiongeze ushuru ili gharama ya maisha iende chini. Serikali inafaa kuzingatia wananchi waliodai kuwatetea ili wapate nafuu."
}