GET /api/v0.1/hansard/entries/1252849/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1252849,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1252849/?format=api",
"text_counter": 257,
"type": "speech",
"speaker_name": "Kaloleni, ODM",
"speaker_title": "Hon. Paul Katana",
"speaker": null,
"content": "Hata Wabunge walio kwa Serikali, imekuwa ni vigumu kwao kuenda mashinani kuonana na watu. Sisi wenyewe hatuna hela mifukoni. Basi tutawasaidia vipi wapiga kura? Dhana hii ya kuwa Wabunge wanapewa pesa za kununua nyumba ni potovu. Ule ni mkopo na tunalipa na riba. Nimechukua mkopo wa nyumba sasa hivi ambao unakatwa katika mshahara. Nyumba hii ninayolazimishwa kulala ni ipi? Mpango huu wa nyumba unafaa kuwa ni kwa hiari. Anayetaka nyumba akatwe pesa katika mshahara ili apate nyumba. Yule aliye na nyumba naye afanye shughuli zingine kama kuezekea na kuongeza biashara yake. Badala ya kupunguza ushuru wa nyumba, wangepunguza ushuru wa mafuta na gharama ya maisha ingeshuka chini."
}