GET /api/v0.1/hansard/entries/125301/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 125301,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/125301/?format=api",
    "text_counter": 672,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Dr. Shaban",
    "speaker_title": "The Minister of State for Special Programmes",
    "speaker": {
        "id": 139,
        "legal_name": "Naomi Namsi Shaban",
        "slug": "naomi-shaban"
    },
    "content": "kidogo kwa sababu Kamati hii ya kufuatilizia Sheria zinazotungwa na Bunge kuwa zitaweza kufuatwa kikamilifu ndiyo mara yake ya kwanza kuanza kazi. Na kwa sababu ndio mara ya kwanza kuanza kazi, tumegundua kwamba Kamati hii iko na mamlaka mazito sana. Sisi Wabunge ndio tumeipatia Kamati hiyo mamlaka hayo. Lakini kwa sababu ndio wameanza kazi, ningependa tu kuwasihi wenzangu ya kuwa katika hali yao ya kuanza kazi, tayari wameanza jukumu zito – jukumu lenyewe ni kukumbusha Serikali kuwa Bunge lipo na Wabunge wanafuata kile ambacho Serikali inatekeleza kwa mujibu wa Sheria zilizotungwa hapa. Bw. Naibu Spika wa Muda, kitambo, kuna wakati mwingine labda sheria zilikuwa zikiminywa-minywa kidogo ili Serikali iweze kutekeleza maswala fulani. Nataka kuwaomba wenzangu, kwa sababu ndio mara ya kwanza kwa swala hili, ningeomba kuwa tuheshimu Gazeti Rasmi la Kiserikali, lakini heshima yenyewe kwanza tumpatie Rais wetu, mhe. Mwai Kibaki. Na heshima yenyewe ni kwa sababu ya vile alivyofanya uamuzi – ijapokuwa yeye ni mbunge wa Othaya – alisahau kuwa Kamati hii inamwangalia na inamweka kwenye darubini kuhakikisha kuwa amefuata sheria zote. Mimi sio mwanasheria, lakini naweza kutunga sheria. Na kwa vile, Bw. Naibu Spika wa Muda, hapa tumejaliwa kuwa na mawakili wengi ambao wanaelewa sheria, na kila anayesoma sheria anaielewa kivyake. Vile vile, nina imani kuwa hata Rais wetu alipoiangalia hiyo sheria, aliisoma na akaielewa kivyake. Pia,Waziri wake wa Maswala ya Haki, Umoja wa Kitaifa na Katiba amesimama hapa na akaeleza na ungeweza kumwelewa kinaganaga kuwa na yeye pia, alivyoielewa ile sheria, imetofautiana kidogo na vile Kamati hii ilivyoielewa hiyo sheria. Bw. Naibu Spika wa Muda, kuambatana na hayo, sisi tuko hapa kwa sababu tumeorodheshwa rasmi kwenye Gazeti Rasmi la Serikali ya Kenya. Wabunge Maalum wako hapa vile vile kwa sababu waliorodheshwa kwenye Gazeti hili. Hakuna njia nyingine ya hao Wabunge kuteuliwa, ila kupitia Gazeti Rasmi la Serikali ya Kenya. Itakuwaje basi kama Wabunge Maalum na Madiwani Maalum--- Hata mimi nilichaguliwa katika Wasilisho la Taveta lakini kama singewekwa katika Gazeti Rasmi la Serikali, kamwe nisingeapishwa ili nitekeleze jukumu langu. Mimi si mwanasheria kama wenzangu ambao wamezungumza. Hata hivyo, naangalia jambo hili kiutu na jinsi nchi yetu ilivyo. Tuko katika wakati gani katika nchi yetu? Majukumu ya Bunge ni mazito sana na Wabunge wamejaribu kubadilisha kanuni"
}