GET /api/v0.1/hansard/entries/125303/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 125303,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/125303/?format=api",
"text_counter": 674,
"type": "other",
"speaker_name": "",
"speaker_title": "",
"speaker": null,
"content": "za Bunge hili. Pia, Bunge limeeleza Serikali ifuate sheria kikamilifu. Serikali imeambiwa isome na ielewe sheria kinaganaga jinsi Bunge linavyoelewa sheria. Naomba Bunge hili la Kumi lifanye hisani tu. Kutokana na kazi anayoifanya Jaji Ringera na wenzake, hakika sisi sote hatuwezi kuwapenda. Hii ni kwa sababu anavuruga na kusaga kila mtu. Huo ndio uweli wa mambo na hivyo ndivyo ilivyo kazi yake. Bw. Naibu Spika wa Muda, tukisimama hapa kumkasirikia yule bwana kwa sababu ya kazi anayoifanya, basi tutakuwa tunakiuka sheria tulizozitengeneza sisi. Kwa hisani yetu, heshima kwa Rais na upendo kwa nchi yetu ya Kenya, ninaomba kwamba--- Waingereza husema kwamba âWarning shotâ imeshapigwa. Bunge linatuangalia sisi tuliomo Serikalini kikamilifu na limetuweka kwenye darubini. Mimi ninaunga mkono juhudi za kurekebisha Ripoti hii. Baadaye, tutasema kuwa tumeipasha habari Serikali vilivyo na lazima ifuate sheria vile ilivyo. Kwa heshima ya Rais, naomba tuondoe suala hilo la kuchanachana Gazeti Rasmi la Serikali ya Kenya kwa sababu tukifanya hivyo, hatutamalizia hapo. Tutaendelea kufanya hivyo kila kunapokucha. Sisi katika Baraza la Mawaziri tumepewa uwezo na Rais kupitia Gazeti Rasmi la Serikali. Kwa mfano, Waziri anaweza kuteua bodi zinazosimamia mashirika ya Serikali. Tukianza kuchanachana Gazeti Rasmi la Serikali kwa sababu hatujaifurahia bodi ambayo labda mimi nimeiteua, basi tutafanya hivyo kila kukicha. Itabidi tuchunge kwa sababu tutajichanachana wakati tutaendelea kuyachana mambo haya. Ninaunga mkono urekebishaji na maoni yaliyotolewa na Bw. Kioni."
}