GET /api/v0.1/hansard/entries/1253074/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1253074,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1253074/?format=api",
"text_counter": 127,
"type": "speech",
"speaker_name": "Mombasa County, ODM",
"speaker_title": "Hon. Zamzam Mohammed",
"speaker": null,
"content": " Asante sana Bwana Spika kwa fursa hii ili niweze kuunga mkono mjadala huu wa leo ama uamuzi utakaotoka hapa leo kuhusu ndugu yetu, Bw. Noordin Haji. Nimemjua Mhe. Noordin Haji tangu nikiwa msichana mdogo wakati walikuwa wanaishi Kakamega na baba yake aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wakati huo. Baba yangu alipofariki, baba yake ndiye aliyenilipia karo ya shule, ndiposa nikamaliza shule ya upili. Tangu ujana wake, Noordin Haji alikuwa mtu tanashati na mchapa kazi. Alipokuwa akihudumu katika ofisi ya NIS kama naibu, alifanya kazi safi sana. Kama tunatafuta wasomi, yeye ni mmoja wao. Pia, ni mwenye bidii. Mimi kama Mama Kaunti wa Mombasa, niliona kazi aliyoifanya akiwa katika ofisi ya NIS alikohudumu mwisho. Ninamtakia kila la heri katika kiti hiki. Ninawaomba Wabunge wamwunge mkono ili aweze kuhudumia Wakenya. Asante sana, Bwana Spika."
}