GET /api/v0.1/hansard/entries/1253100/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1253100,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1253100/?format=api",
"text_counter": 153,
"type": "speech",
"speaker_name": "Likoni, ODM",
"speaker_title": "Hon. Mishi Mboko",
"speaker": null,
"content": " Asante sana, Mhe. Spika. Ninaunga mkono kuteuliwa kwa Bw. Noordin Haji katika kitengo cha Huduma ya Ujasusi wa Kitaifa. Ninamuunga mkono kwa sababu amefuzu katika tajiriba ya kielimu, na pia ana uzoefu na uweledi wa mambo ya usalama na ujasusi. Amefanya kazi katika vitengo tofauti tofauti. Tunajua atatuwezesha kupunguza misimamo mikali ile tunaita extremism na mambo ya AlShabaab. Tunajua kuwa amefuzu katika mambo ya ujasusi na pia hana dosari katika uongozi na uadilifu. Vile vile, hajawahi kuhukumiwa kwa shutuma yoyote ya kijinai ama katika mambo ya uhalifu."
}