GET /api/v0.1/hansard/entries/1253211/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1253211,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1253211/?format=api",
    "text_counter": 264,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Nakuru County, UDA",
    "speaker_title": "Hon. Liza Chelule",
    "speaker": null,
    "content": " Ahsante sana, Bwana Spika kwa kunipa nafasi niunge mkono wenzangu ambao wameunga hawa watendakazi wawili, Bw. Rutto na huyu msichana. Wawili hawa wako tayari kufanya kazi katika nchi yetu ya Kenya. Sisi sote tunamjua aliyekuwa Mhe. Isaac Rutto wa Bomet. Wakati mwingine alichaguliwa kuwa Mjumbe na wakati uliofuata akachaguliwa kuwa Gavana wa Bomet. Kazi ambayo alifanya ni nzuri sana. Huyu ni kiongozi ambaye tunaelewa kwamba alikuza mambo ya ugatuzi sana. Ni kiongozi ambaye alitatua shida kule Bomet. Naelewa kuna wakati mmoja kulikuwa na jamii mbili zilizokuwa zimekosana upande wa Borabu. Yeye ndiye aliyeongoza mazungumzo kati ya jamii hizo mbili. Huyu ni kiongozi ambaye anaonekana kutokuwa na mpaka kwa kazi yake. Sisi kama Wajumbe, tunaunga mkono kiongozi ambaye atawaunganisha Wakenya. Tunajua kwamba atafanya kazi hii kwa njia nzuri. Kwa niaba ya watu wa Nakuru, na kwa niaba yangu mwenyewe, ninaunga mkono Hoja hii ili Mhe. Rutto apate kazi hiyo."
}