GET /api/v0.1/hansard/entries/1253227/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1253227,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1253227/?format=api",
    "text_counter": 280,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Likoni, ODM",
    "speaker_title": "Hon. Mishi Mboko",
    "speaker": null,
    "content": " Asante Mhe. Spika. Naunga mkono uteuzi wa Caroline na Isaac Kiprono Rutto ili waweze kuhudumu katika Tume ya Huduma za Mahakama. Uteuzi huu umeweza kuzingatia sera ya jinsia na sisi kama akina mama tunashukuru sana. Nilimjua Mhe. Isaac Rutto alipokuwa Mbunge na gavana. Utendakazi wake hauna ubaguzi. Yeye ni kiongozi ambaye haogopi na huzungumza hisia za ukweli kutoka moyoni mwake. Dada yetu, Caroline, pia ameweza kufuzu vizuri katika tajriba ya kielimu. Hana dosari yoyote katika mambo ya uongozi na uadilifu. Watu hawa wawili wakiwa katikaTume hii, ni muhimu sana wahakikishe kwamba mahakama inatekeleza wajibu kwa njia ya kumsaidia Mkenya, haswa katika mambo ya kisheria na hukumu. Hii ni kwa sababu tumeona dhuluma nyingi sana zikifanyika. Watu wengine wanahukumiwa pasipo na makosa. Walio na makosa wanatumia njia ambazo si sawa ili kuepuka hukumu. Nina amini kwamba wateuzi hawa wawili, haswa Isaac Kiprono Rutto, ambaye kwa kiingereza wanasema ni no-nonsense man; ni kiongozi ambaye akilenga amelenga na akisema amesema, haogopi, hatishwi wala hatingishiki… Kwa hivyo, tunajua kwamba Tume ya Huduma za Mahakama itaweza kuongozwa kwa njia ya kufuata mujibu wa Katiba ya Kenya. Hivyo basi, Mkenya ataweza kupata haki yake bila kudhulumiwa. Mhe. Spika, ninaunga mkono."
}