GET /api/v0.1/hansard/entries/1254897/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1254897,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1254897/?format=api",
    "text_counter": 124,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Kinyua",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 13202,
        "legal_name": "John Kinyua Nderitu",
        "slug": "john-kinyua-nderitu-2"
    },
    "content": "Ukitembea sehemu nyingi, utapata vijana wameketi katika mitaa wakiwa walevi chakari. Ni vizuri pombe haramu zipigwe vita kama tunataka kupiga hatua kimaendeleo. Wakati mambo haya yanapofanywa, ni vizuri vijana wetu watafutiwe kazi. Hii ndio sababu serikali inasema ni vizuri nyumba zijengwe ili vijana waweze kupata ajira. Vijana wengi wanakaa mitaani na mijini bila kazi na wanakunywa pombe; ni vinyo kila mahali."
}