GET /api/v0.1/hansard/entries/1254905/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1254905,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1254905/?format=api",
    "text_counter": 132,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Madzayo",
    "speaker_title": "The Senate Minority Leader",
    "speaker": {
        "id": 679,
        "legal_name": "Stewart Mwachiru Shadrack Madzayo",
        "slug": "stewart-mwachiru-shadrack-madzayo"
    },
    "content": "Tunajua ya kwamba ni makosa sana kusumbua wale watu wakiwa katika hali zao za starehe. Watu wakiwa katika hali zao za starehe katika bar zile kubwa kubwa hawasumbuliwi kama wale wadogo wanaoketi katika zile bar ndogondogo kama zile ziliko Kakamega; wale wanakunywa busaa, muratina na pombe zingine. Sheria inafaa izingatiwe kwa hao watu pia. Bw. Spika, pombe yote inasafarishwa kwa boda boda. Mimi natoka eneo la Kaunti ya Kilifi. Wazee hukaa chini sababu ile pombe ya mnazi imebarikiwa sana. Ikiwa ni harusi, mazishi na mazungumzo ya aina yoyote ni lazima iweko. Katika zile hali, wazee hukaa na hata kubariki kijana anayeenda kuoa na hiyo. Mara nyingi tunaona askari wakitumia hiyo sheria vibaya kwa sababu wanaenda kufurusha wale halafu wanaacha wale mabwenyenye. Kazi yao ni kutafuta mashamba kwa wale wamepata amri za bandia kutoka kortini, kuvunjia watu nyumba ama kufanya vitu vyo vyote vya kufukuza wananchi katika hali yao ya starehe. Kuna umuhimu katika ile Hoja aliyosema Sen.Wafula, kwamba wale watu wote wanaokuwa vijijini na starehe zao hawana fujo. Pia kuna wale waendeshaji boda boda wanachukua kile kinywanji na kusafirisha, wakifikisha kule na kupata riziki zao za kusaidia nyumbani. Ni muhimu kuwe na sheria mwafaka ambayo inaweza kuwalinda. Bw. Spika, naunga mkono Sen. Wafula vile alivyosema na ninatarajia kwamba ile Kamati itakayokwenda itazingatia suala hilo. Ahsante."
}