GET /api/v0.1/hansard/entries/1255153/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1255153,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1255153/?format=api",
"text_counter": 380,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Mwaruma",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13223,
"legal_name": "Johnes Mwashushe Mwaruma",
"slug": "johnes-mwashushe-mwaruma"
},
"content": "Asante, Bi. Spika wa Muda, kwa kunipa hii fursa ili kuchangia Mswada huu. Kwanza nashukuru Seneta Mteule aliyeleta huu Mswada, Sen. Mutinda. Mswada huu unahusu wahudumu wa kilimo. Si mara ya kwanza tumekuwa na wahudumu wa kilimo. Wamekuwa tangu zamani nikiwa mtoto mdogo. Tulikuwa na Serikali ya kitaifa, walikuwa wakisaidia sana wakulima wetu. Ile kazi walifanya ilikuwa kazi kubwa sana. Afisa hao walisaidia kuendeleza kilimo katika jamii. Hiyo huduma ilififia na kwa saa hizi haieleweki vizuri kama hawa wahudumu wa kilimo bado wako ama hawako."
}