GET /api/v0.1/hansard/entries/1255155/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1255155,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1255155/?format=api",
"text_counter": 382,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Mwaruma",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13223,
"legal_name": "Johnes Mwashushe Mwaruma",
"slug": "johnes-mwashushe-mwaruma"
},
"content": "Ninakumbuka kuna wakati nilikuwa mkulima miaka 20 iliyopita. Nilipanda nyanya nyingi sana kama ekari tatu. Ilikuwa ni nyingi kulingana na mimi nikiwa kijana mdogo. Nilitafuta mhudumu wa kilimo na ilichukua siku mbili yeye kuja sababu nyanya zangu zilikua zimepata ugonjwa siuelewi, uliokuwa kama blight. Bi. Spika wa Muda, alipokuja baada ya siku tatu, nilipoteza nyanya nyingi ilhali makisio yangu nilikua nipate kama tani tano. Huyo mhudumu alikua mgonjwa na alikua mmoja na kwa kuchelewa kwake, nilivuna nusu tani peke yake. Lazima niseme hawa wahudumu ni wa muhimu sana. Nashukuru Sen. Mutinda kwa kuona kwamba ni vyema aweke mswada ambao unaleta sera na sheria ya kuangazia hawa wahudumu. Malengo ya huu Mswada ni kwamba ya kwanza, ameangazia vile Serikali za Kitaifa na kaunti zitakavyo shirikiana ili kuhakikisha ya kwamba hii huduma ya kilimo kwa hawa wahudumu imewekwa vizuri zaidi. Kwa kuweka wahudumu wa kilimo vizuri, basi kutaenda kutokea mapato ya juu zaidi. Bi. Spika wa Muda, kwa sasa hivi, kulingana na vile Sen. Methu amesema, yale mavuno tunayopata kwa mifugo na kilimo yamekua yakididimia vile miaka inavyoenda. Ukipanda ekari moja ya mahindi unatakikana kupata kama magunia ishirini. Lakini kwa sasa hivi na kwa sababu ya kukosa huduma ya hao wahudumu, unaeza pata magunia matano au manane. Kuna ile tunaita Gross Domestic Product (GDP) inashuka chini. Ukiangalia kwa upande wa mifugo, tukiwa na wahudumu, wanatuelezea mbinu nzuri za ukulima. Kwa mfano kwa kufuga ngombe. Yale maeneo ninayotoka Wundanyi, tunafuga ng’ombe. Kitambo ukiwa na ng’ombe angetoa lita 20 au 30 na kadhalika. Lakini, kwa sababu ya kukosa hizi huduma na ushauri wa hawa wahudumu, unapata yale mazao yanadidimia. Bi. Spika wa Muda, kitu moja wakulima wetu walikua wanafundishwa ni kuweka wanyama wasikae pamoja na wazazi wao ndio wasizae pamoja. Kwa Kizungu inaitwa in-breeding . Mswada huu ukipita vizuri na kuwe na wahudumu basi mazao yataenda kuendelea. Mswada huu pia unaangazia lengo la kuwa na utafiti ambao ni kiungo muhimu kabisa katika kuongeza mazao sababu tutapata breeding katika mazao yetu na mifugo yetu. Ni lazima tuekeze kwa utafiti. Lengo lingine ni kwamba hao wahudumu hawajapatiwa fedha za kutosha. Kilimo kimegatuliwa lakini huu Mswada unaangazia maswala ya vile kutakua na kushirikiana kati ya Serikali ya kitaifa na ya kaunti ili kuhakiki kwamba hii huduma ya wahudumu wa kilimo inapatiwa pesa zaidi kwa upande wa utafiti. Tumeona kwamba Mswada huu unapendekeza kuwe na huduma ama National"
}