GET /api/v0.1/hansard/entries/1255159/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1255159,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1255159/?format=api",
"text_counter": 386,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Mwaruma",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13223,
"legal_name": "Johnes Mwashushe Mwaruma",
"slug": "johnes-mwashushe-mwaruma"
},
"content": "Ninakubaliana na wasemaji wengine ya kwamba zamani tukiwa wadogo, kulikua na shule za kufunza wakulima au Farmers Training Centres. Saa hizi nyingi zimetelekezwa, zikaachwa na haziendelei. Labda hio bodi ya National and CountyExtension Service inatakiwa iangazie kuwa na zile shule mashinani ili kuhakikisha ya kwamba wakulima wetu wanafunzwa mbinu totafuti tofauti za ukulima. Bi. Spika wa Muda, nakuabaliana na huu Mswada sababu kilimo kimegatuliwa na kuna huduma fulani zinatakikana zifanyike Serikali ya kitaifa. Kwa mfano, Waziri wa Serikali ya kitaifa anatakikana kuandika sera na sheria za kuangazia ama kuhakikisha hii huduma kwa wakulima iko sawa kwa kaunti zote 47. Je, serikali za kaunti zinafaa kufanya nini? Wanafaa kuangazia na kuweka bajeti za kutosha ili kuhakikisha kuwa huduma za jamii zimegatuliwa pia katika kata."
}