GET /api/v0.1/hansard/entries/1255162/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1255162,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1255162/?format=api",
    "text_counter": 389,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. (Dr.) Murango",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 13585,
        "legal_name": "Murango James Kamau",
        "slug": "murango-james-kamau"
    },
    "content": "Asante, Bi. Spika wa muda, kwa kunipa nafasi hii nichangie Mswada huu wa kuboresha kilimo ulioletwa na Sen. Tabitha Mutinda. Niruhusu nirudi nyuma kidogo wakati nilipokua mtoto kule kijijini. Nilipokuwa mtoto, tulikuwa tunatazama magari mengine madogo yaliyokuwa yakiitwa Suzuki. Maafisa wa kuboresha ukulima katika jamii walikua wanazunguka kila siku na magari yale. Ng’ombe walikua wanaelekezwa kwenye zizi kando ya barabara na ulipotaka mbegu ulizipokea. Haya yote yalifanywa ili kuboresha mbegu za ng’ombe. Huduma ile ilikua inapatikana katika kaunti zote. Haya ni mambo ambayo sijawahi ona katika kaunti nimetoka. Nauunga huu Mswada mkono. Kuna umuhimu mkubwa wa kuweka maafisa wa kutosha ili waeneze huduma bora. Mwaka huu, Kaunti ya Kirinyaga imetoa mazao mengi ya kahawa nchini. Tunakuza pia majani chai. Tunazo shamba kubwa sana za kukuza mchele kwa njia ya umwagiliaji maji. Wakulima hawa wanafaa kupewa huduma za kilimo ya kuwaelimishwa aina ya mbegu ambayo ni mzuri kupanda. Wanafaa kuelezwa ni mikakati gani wataweka ikiwa udongo umezidi asidi au PH. Wakulima wale bado wanalia. Ni muhimu hiyo ifanywe kwa sababu ugatuzi upo. Kaunti zinafaa kuongeza wale maafisa ili wahudumie wakulima katika sehemu zile. Wakati uliopita haukuwa na shida nyingi. Ng’ombe na mbuzi walikua na afya nzuri. Nilipopitia katika mji wa Kutus juzi, nilipata “kuku mbuzi”. Hawa ni mbuzi ambao wamepungua kilingo na kutoshana na jogoo. Katika kilimo kama ya kahawa, panafaa kuwa na maabara maalum ya wale maafisa ili waupime ule udongo bila kuwalipisha wakulima. Hii itawapa wakulima ufahamu wa kile ambacho wanafaa kuongeza katika mashamba yao. Ukosefu wa lishe bora katika jamii unachangiwa sana na kukuza mimea kwa udongo unaokosa virutubisho vinavyohitajika katika mwili wa binadamu. Najua kuna pesa ambazo zinafaa kwenda katika Kaunti. Hizo pesa zinafaa kutumika vizuri ili ziwapatie wakulima huduma bila malipo yoyote. Sio huduma pekee,"
}