GET /api/v0.1/hansard/entries/1255164/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1255164,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1255164/?format=api",
"text_counter": 391,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. (Dr.) Murango",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13585,
"legal_name": "Murango James Kamau",
"slug": "murango-james-kamau"
},
"content": "pia mitambo ya kisasa. Huduma hizi zinafaa kuwa katika ugatuzi ili wakulima waepuke kusafiri hadi maabara ya Serikali Kuu ambayo yako mbali ili kupata huduma. Hivi karibuni nilizuru kiwanda cha kusaga kahawa ya Kibirigwi. Wanapambana sana kule. Wameajiri mtu ambaye wanamlipa wenyewe ili kuboresha miche ya Kahawa, ile ili watoe mazao mengi ya kahawa ya Arabica. Kama Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Kilimo, Mifugo, Uvuvi na Umwagiliaji Maji, nauunga mkono Mswada huu ili ufaidi watu wetu. Nachukua nafasi hii kushukuru Serikali Kuu kwa sababu nimekuwa nafuata kwa karibu bei ya mbolea ya ruzuku ambayo inaenda kulima mchele kule kata ya Mwea. Kilio nilichotoa kimefika na ifikapo kesho au kesho kutwa wakulima watapata ile mbolea kwa bei ya Kshs2,000 sio Kshs3,500. Hii ni mbolea wanayoita ya sukari au sulphate ofammonia . Kwa hayo machache, naunga mkono Mswada huu. Asante."
}