GET /api/v0.1/hansard/entries/1255183/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1255183,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1255183/?format=api",
"text_counter": 410,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Faki",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13211,
"legal_name": "Mohamed Faki Mwinyihaji",
"slug": "mohamed-faki-mwinyihaji-2"
},
"content": "Asante Bi. Spika wa Muda, kwa kunipa fursa hii kuongeza kauli yangu katika Mswada ambao umeletwa bungeni na Sen. Tabitha Mutinda. Bi. Spika wa Muda, Mswada huu wa maafisa wa nyanjani wa ukulima na ufugaji ni Mswada ambao utasaidia pakubwa kuongeza mazao katika sehemu ya ukulima na vile vile pia mazao katika sehemu ya ufungaji wa wanyama katika nchi yetu ya Kenya. Kwa sasa ijapokuwa huduma za ukulima na ufugaji zimegatuliwa, tukiangalia ile bajeti ambayo inatolewa katika nyanja hizo, katika kaunti zetu ni ndogo sana. Ni kiasi ambacho hakiwezi kufanya jambo lolote la kuweza kusaidia ukulima katika sehemu zile. Kwa mfano tukiangalia Mombasa, nimeona kwamba ni asilimia ndogo sana ya bajeti ambayo inakwenda katika ukulima. Ijapokuwa wengi wanasema kwamba Mombasa ni mji na kwamba hakuna ukulima unaofanyika, kuna sehemu nyingi kama vile Mwakirunge na Likoni ambapo wananchi wanafanya ukulima. Iwapo hawataweza kusaidiwa na maafisa kama hawa, basi kilimo kitaweza kufa kabisa katika sehemu zile. Kitaifa tumeona pia kwamba pesa zinazopelekwa katika taasisi za utafiti kama vile Mtwapa na Msabaha, tumeona kwamba zinazidi kupungua. Kwa mfano, kwa mwaka huu wa 2022/2023 hakuna pesa zozote ambazo zilitolewa kwa ufadhili wa utafiti kuhusiana na minazi na mikorosho katika sehumu zile. Ilhali hiyo ndio mazao makubwa ambayo yanatengemewa katika sehemu za Pwani ili kuongeza mapato ya wakulima. Mimi nina shamba ndogo kule sehemu ya Kwale. Juzi tuliitwa na Kaunti ya Kwale kuenda kupewa mimea. Tulipewa miche ya minazi na vile vile mikorosho. Jambo la kusikitisha ni kwamba mtu ambaye ana shamba la ekari kumi anapewa miche miwili ya minazi na mikorosho. Bi. Spika wa Muda, hiyo ni kama kejeli. Lakini pia hatuwezi kulaumu sana kwa sababu ya hizo fedha ambazo zimetolewa na serikali ambazo zimeweza kufadhili ukulima na utafiti katika sehemu zile. Jimbo la Pwani lina uwezo wa kuuza kila aina ya mimea. Tukizungumzia mchele, mchele unalimwa sehemu za Kwale, Kilifi na Tana River. Tukiangalia masuala ya uvuvi, tuna sehemu nyingi ambazo tunaweza kufanya uvuvi wa kisasa ile ambayo wazungu wanaita aquaculture. Sehemu ya Tana River kuna ardhi ambayo inashikana na bahari na vile vile Mto Tana ambao unaweza kutumika kuzalisha samaki ambao wataweza kusaidia kukimu mahitaji ya wananchi na chakula katika taifa letu. Bi. Spika wa Muda, ni lazima tuunge mkono Mswada huu na tuhakikishe kwamba kaunti zetu zinatoa ruzuku ili ukulima na ufugaji unakuzwa katika sehemu hizi. Kwa mfano, nchini Uganda kuna utafiti hadi wa mihogo. Mihogo ni cassava . Sasa hivi, mihogo mingi katika soko za Kaunti ya Mombasa, inatoka nchini Uganda na pia Kaunti ya Busia."
}