GET /api/v0.1/hansard/entries/1255185/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1255185,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1255185/?format=api",
    "text_counter": 412,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Faki",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 13211,
        "legal_name": "Mohamed Faki Mwinyihaji",
        "slug": "mohamed-faki-mwinyihaji-2"
    },
    "content": "Kuna mambo mengi sana ambayo tunaweza kuzungumzia lakini tunachunga muda. Mswada huu utachangia pakubwa kuongeza mapato ya wakulima na ya kaunti zetu. Vile vile, itazuia uagizaji wa chakula kama mchele, ngano na vinginevyo kutoka mataifa mengine. Bi. Spika wa Muda, hapo zamani, mchele mzuri kama Basmati ulikuwa unatoka Mwea. Kwa wale ambao wanakumbuka, kulikuwa na Mwea Pishori ambayo ilikuwa inauzwa mpaka soko za nje. Lakini hivi sasa, mchele wetu unatoka Pakistan kwa sababu ukulima wetu umezorota miaka nenda, miaka rudi. Ninaunga mkono Mswada huu."
}