GET /api/v0.1/hansard/entries/1255593/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1255593,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1255593/?format=api",
"text_counter": 332,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. (Dr.) Murango",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13585,
"legal_name": "Murango James Kamau",
"slug": "murango-james-kamau"
},
"content": "Asante, Bw. Spika wa Muda kwa kunipa hii nafasi kumuuliza Waziri wa Kilimo swali. Yangu sio mengi. Kwanza naomba nikushukuru Mhe. Waziri. Waswahili husema, mghala muue na haki yake mpe. Kwanza ninakushukuru kwa ile kazi umefanya kuhusu mbolea. Leo nimetoka Mwea na ile shida ambayo ilikuwa kwa wakulima, umeitatua kwa muda mfupi sana. Kwa sasa, wakulima wamefurahi. Jambo dogo tuu ni kwamba tufunge maneno ya fertilizer aina ya 1717 na 23, na tupange maneno ya ndege kwa sababu ya wale Quela."
}