GET /api/v0.1/hansard/entries/1255594/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1255594,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1255594/?format=api",
"text_counter": 333,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. (Dr.) Murango",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13585,
"legal_name": "Murango James Kamau",
"slug": "murango-james-kamau"
},
"content": "La pili ni mambo na mchele. Umetupatia mbolea. Tunalima mchele Mwea, Bunyala, Ahero na Bura na tutalima mchele wa kutosha. Kwa hivyo, ninaomba wakati mnafanya uamuzi wa kununua mchele kutoka nje, mhakikishe ya kwamba ule mchele ambao tutalima kwa hiyo mbolea ya ruzuku, mmeuchukua wote ili wakulima wafurahie. Kuna kiwanda ambacho kinaitwa MRGM. Kilichukuliwa mchele na KNTC, ambayo ninajua haiko kwa Wizara yako. Lakini, toka Desemba hadi leo, hawajalipwa pesa zao. Wameanza kukopa pesa ili wapande mchele kwa sababu huu ni msimu wa upanzi. Ninaomba pia uzungumze na Waziri wa Kilimo pia, ili walipwe ndio wasikope pesa ama pembejeo za kushughulikia mchele."
}