GET /api/v0.1/hansard/entries/1257682/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1257682,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1257682/?format=api",
"text_counter": 133,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Munyi Mundigi",
"speaker_title": "",
"speaker": null,
"content": "Bw. Spika, ninaunga Mswada huu ambao Seneta wa Kitui ameleta kuhusu ndengu. Kaunti ya Embu ni mojawapo ya zile kaunti zinalima ndengu kama kaunti 35 zinginezo. Mbeere South na Mbeere North, inapakana na Kitui. Bei ya ndengu iko chini sana. Ukienda kwa supermarket, Uganda, India au hoteli zetu utakuta ndengu. Kwa hivyo, ninaunga mkono mambo ya kilimo ya mmea huu. Ili tupate kilimo bora, lazima tuwe na maji ya irrigation . Serikali pia itupee dawa na fertilizer kwa bei ya chini. Ikifanya hivyo, tutaendelea vyema na tutaboresha kilimo. Mkulima akipanda ndengu, atavuna baada ya miezi mitatu au minne. Pia, shamba lisilo na mbolea nyingi linapo pandwa litahitaji maji kidogo, na mkulima atavuna ndengu. Ninaunga mkono kilimo cha ndengu. Serikali ikitusaidia tutapata bei nzuri. Tunaomba Serikali itutafutie soko za kuuza nchi za ng’ambo."
}