GET /api/v0.1/hansard/entries/1257849/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1257849,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1257849/?format=api",
"text_counter": 300,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Kinyua",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13202,
"legal_name": "John Kinyua Nderitu",
"slug": "john-kinyua-nderitu-2"
},
"content": "kongole kwa sababu wakulima wa ndengu walikuwa hawajulikani. Nimewasikiza Maseneta wote walioongea na ni kama hawakufahamu ndengu kwa lugha ya kingereza ni nini. Kwa hivyo, Sen. Wambua nakupongeza kwa sababu wakulima walioonekana ni wa kahawa, majani chai, mahindi, pareto na pamba. Ninakushukuru kwa kuwapa hadhi wakulima wa ndengu. Nikianglia Mswada huu kwa undani, Sen. Wambua amependekeza kuwa ukulima wa ndengu utakuwa kilimo biashara. Mambo yote ambayo yametajwa hapa yanazingatia kuleta gharama nafuu ya ukulima wa ndengu. Ni vizuri ijulikane wazi kuwa anasisitiza ni mbegu gani zitakazotumiwa. Mbegu za hali ya juu ambazo utafiti umefanywa tayari. Sen. Wambua anasema ya kwamba ni lazima mbegu ziidhinishwa. Anaendelea kusema vileviel mbolea iangaliwe. Anaendelea kusema hata mchanga katika mashamba ya wakulima unaangaliwe ili kujua ni mchanga upi unaofaa kutumika katika ukuzaji wa ndengu. Hakomei hapo, anaendelea kusema tuwe na mikakati ya kutosha ya kuhakikisha kwekwe zimeangamizwa mashambani. Anaonyeshana vizuri vile hayo mambo yote yanapaswa kufanywa."
}