GET /api/v0.1/hansard/entries/1257855/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1257855,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1257855/?format=api",
"text_counter": 306,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Kinyua",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13202,
"legal_name": "John Kinyua Nderitu",
"slug": "john-kinyua-nderitu-2"
},
"content": "Bw. Spika wa Muda, nasimama kuunga mkono Mswada huu. Hili ni jambo nzuri, hasa katika Kaunti ya Laikipia. Tukizangatia mambo haya yote anayopendekeza katika Mswada huu kila kaunti ikiyangalia kwa undani, basi sisi sote tutafaidika. Wakulima wa Kaunti ya Laikipia wanaweza kuwatembelea wakulima wa Kaunti ya Kitui na kuona jinsi wanavyokuza ndengu zao. Mchanga ni upi uko pale katika Kaunti ya Kitui. Sisi katka Kaunti ya Laikipia tuna wanao wanasayansi ambao wanaweza kutushauri kama tunaweza kukuza ndengu. Wakulima wa ndengu katika Kaunti ya Laikipia watajulikani. Yeye amesema wakulima wa ndengu nchini Kenya haijulikani. Hili litakuwa ni jambo nzuri kwa sisi kusoma kutoka Kaunti ya Kitui. Ikiwa utaupitisha Mswada huu kuwa sheria utawasaidia wakulima wa ndengu. Sisi wafugaji wa ng’ombe tunaweza tukaiga hii sharia. Sen. Wambua amezungumzia utafiti, hata sisi tunapaswa tufanye utafiti ili tujue ni mbegu gani nzuri ya ndume ambayo tunaweza tukawa nayo. Tufanye utafiti ni chumvi gani inaweza ikatumika katika Kaunti ya Laikipia ili kuongeza mavuno yetu maradufu. Bw. Spika wa Muda, tukizingatia vile alivyosema Naibu wa Rais na Mhe. Thang’wa ataniunga mkono kwa sababu hili jambo la majani chai na kahawa limekuwa na hawa wakora ambao kazi yao ni kuvuna ambapo hawakupanda. Hili ndilo swala nyeti ambalo najua Sen. Wambua anazingatia ndio tuweze kuondoa hawa brokers na cartels. Watu hao, hawana shamba lolote na hawajalima pahali popote, lakini wanafaidika kutoka na jasho la wakulima wa majani chai na kahawa. Hawana chochote wanachokifanya. Kazi yao kubwa ni kukaa na kungoja wakulima wakuze mazao yao na kuwalaghai. Mimi naweza kuwalinganisha na fisi. Kazi yake ni kumfuata mtu anaangalia kama mkono unavyoenda akingoja uanguke. Hawalimi, hawafanyi chochote lakini wao ni kungoja kuwalaghai wakulima kwa sababu hawana mahali pa kuuza mazao yao. Nashukuru Sen. Wambua kwa sababu ameangazia mambo ya masoko ya ndengu. Sina shaka rohoni yangu kuwa Sen. Wambua alichaguliwa mara ya pili kwa sababu ya kuwatetea wakulima wa ndengu. Mswada huu ukipita, sitaki kusema lakini kwa sababu macho yangu huona mbali pengine Sen. Wambua atakuwa Gavana wa Kaunti ya Kitui. Ni maombi yangu kwa vile Mungu. Mungu si athumani. Bw. Spika wa Muda, naunga mkono Mswada huu. Namwambia Sen. Wambua, baada ya sisi kupitisha, afuatilie vizuri wale wakulima wa ndengu pale Kaunti ya Kitui, ndiposa wawe funzo kwetu sisi ambao tumetoka sehemu zile zingine ambazo hatukuzi ndengu. Pengine tunaweza tukatumia Mswada huu kujua ni vipi hata sisi tunaweza tukakuza ndengu na hata mimea mingine katika kaunti zetu, hasa Kaunti ya Laikipia. Tujue tunaweza kutumia sheria hizi tuweze kuwasajili wakulima wetu, kuwapatia mbolea na kuweza kuwatafutia soko ya mimea yetu ili waweze kupata faida kwa mimea ambayo wamepanda. Bw. Spika wa Muda, nashukuru na ninaunga mkono Mswada."
}