GET /api/v0.1/hansard/entries/1259071/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1259071,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1259071/?format=api",
    "text_counter": 1192,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Lamu East, JP",
    "speaker_title": "Hon. Ruweida Mohamed",
    "speaker": {
        "id": 2100,
        "legal_name": "Shariff Athman Ali",
        "slug": "shariff-athman-ali"
    },
    "content": " Ni muhimu hii pesa ije hata kama ni kidogo. Bora tuipate itumike vizuri. Hii pesa muda wake usije ukaisha kabla haijatumika. Sisi miradi yetu ikija kule iwe ni miradi itakumbukwa na hata vizazi vijavyo. Kuna sehemu nyingine kama vile Lamu Mashariki ambayo ilipata pesa hii ya usawazishaji. Pesa ilikuwa ya kujenga barabara lakini hiyo barabara tukiitafuta leo haiko. Zaidi ya Ksh1 milioni zilitumika. Tunaomba pesa hii itumike vizuri. Haki pia itendeke. Kila Wadi ipate haki yake. Isiwe wadi nyingine kama Basuba Ward inaambiwa kuna mambo ya usalama basi siku zote haifanyiwi miradi kwa sababu ya mambo ya usalama. Ikiwa hivyo, siku zote basi sehemu zisizo salama hazitawahi kupata maendeleo. Zitabakia vilevile. Basi kama ni hivyo waamue watugawanye watupeleke upande mwingine wa Somalia. Au kama ni Kenya, miradi ifike kule hata kama ni Boni Forest. Ahsante Bw. Spika wa Muda."
}