GET /api/v0.1/hansard/entries/1259163/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1259163,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1259163/?format=api",
    "text_counter": 65,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Madzayo",
    "speaker_title": "The Senate Minority Leader",
    "speaker": {
        "id": 679,
        "legal_name": "Stewart Mwachiru Shadrack Madzayo",
        "slug": "stewart-mwachiru-shadrack-madzayo"
    },
    "content": " Asante Bw. Spika. Kwanza nampa ndugu yangu, Sen. Cherarkey, kongole kwa kuleta hii Kauli. Wanaspoti wanapokuwa katika ujana wao, wanaleta sifa kubwa nchini, tukielewa ya kwamba kila mwanaspoti katika nchi za ulaya amewekewa insurance ambayo inaweza kumuangalia kukitokea ajali ya aina yoyote. Jambo la kusikitisha ni kwamba hapa kwetu wanaspoti hatuwapi kipau mbele. Baada ya kuleta sifa, ifikapo uzeeni wao, ni hatua gani itachukuliwa ili kuona mwanaspoti anaishi vizuri? Yule dada aliyetuletea sifa kubwa nchini, Faith Kipyego, alifanya kitendo ambacho hakuna binadamu mwingine ameweza kukifikia. Hii ni sifa kubwa sana ya Kenya. Nawashukuru Wakenya ambao walitimiza azma yake ya kununulia babake gari. Baada ya kufaulu katika kutimiza ile ndoto yake, kuna wanakenya ambao wapata motisha kuwa ndoto zao wanaweza kamilisha. Kitendo hicho kilikuwa cha maana sana ili kumpa nguvu dada yetu. Baada ya hapo, dada huyo alituahidi kuwa katika zile mbio zinazofuatia atatuletea sifa zaidi. Hili ni jambo ambalo tunapaswa tulipatie kipau mbele. Upande wa Pwani kulikuwa na wachezaji wakubwa wa kandanda; Ali Kajo, Sungura, Kadenge, Mohamed"
}