GET /api/v0.1/hansard/entries/1259169/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1259169,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1259169/?format=api",
    "text_counter": 71,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Kinyua",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 13202,
        "legal_name": "John Kinyua Nderitu",
        "slug": "john-kinyua-nderitu-2"
    },
    "content": "Asante, Bw. Spika. Naunga mkono Kauli iliyoletwa na Sen. Cherarkey. Ninawapa kongole wanariadha na wanamichezo wetu ambao wanaleta sifa katika nchi yetu. Faith, tulimuona katika uga akikimbia. Kila mtu alimshabikia. Kama vile Viongozi wa Walio Wengi na Walio Wachache walivyosema, wale ambao wameletea nchi yetu sifa ni vizuri waje kwenye Seneti. Tusiwe tunawaita wale ambao tunataka kuwauliza maswali pekee. Tunapaswa kuwaalika pia wale ambao tunapaswa kuwapa kongole na sifa. Hata wale hawakufanya vizuri leo, ni vizuri tuwape motisha kwa sababu wanawezakufanya vizuri leo, lakini kesho wanaweza kufanya vizuri zaidi. Tusiwe tunawashabikia sana wale waliofanya vizuri tu, wale wengine wangefanya vizuri isipokuwa ya sababu tofauti. Naunga mkono matamshi ya Kiongozi wa Walio Wachache. Bw. Spika, wengine waliokuwa wamefanya vizuri sana ni kama Rudisha aliyekuwa mkimbiaji na mwana dada wa dondi aliyefanya vizuri lakini sasa anaishi katika hali ya uchochole. Alipokuwa anasifa, kila mtu alimshabikia. Kwa wakati huu, ni wagonjwa na wakenya wamenyamaza kimya. Kwa hivyo, kunapaswa kuwa na sheria nzuri ambayo itakuwa ikiwalinda ndio mtu akifika maisha yake ya usoni, wakati pengine hawezi kukimbia ama amepata majeraha kama vile Rudisha alivyopata jereha katika mguu wake na hawezi kimbia, aweze kupata hali yake ya kujikimu. Hata hivyo, nimesikia watu wengine wakisema wanaspoti wetu waweze kufunzwa jinsi ya kuekeza hela wanazozipata lakini ni vizuri tulete mswada ambayo itawalinda. Bw. Spika, kuna taarifa ambazo zimekuwa zikiletwa hapa. Nakumbuka Mheshimiwa Sakaja alileta mambo ya moto uliotokea Gikomba na Toy Market. Inakuwa ni kama kawaida taarifa zinaletwa hapa katika Seneti hii, zinasomwa na baada ya kusomwa hakuna jambo lolote linalofanyika. Linakuwa sisi ni kusoma tu taarifa na muda unaendelea. Nilimsikiza Gavana Sakaja akisoma hizo taarifa za moto ambayo inatendeka na hakuna jambo lolote limetendeka. Bw. Spika, unakumbuka vile vile hata kuna watoto wetu walioko katika nchi za Ugaibuni na wamekuwa katika shida hizi hizi. Kumeletwa taarifa hapa na huwa zinapelekwa katika Kamati, lakini baada ya taarifa zenyewe kuletwa katika Kamati nawao kufanya utafiti, hakuna jambo lolote linafanyika katika Seneti. Serikali nayo halichukulii jambo hilo kwa uzito unaofaa."
}