GET /api/v0.1/hansard/entries/1259273/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1259273,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1259273/?format=api",
"text_counter": 175,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Madzayo",
"speaker_title": "The Senate Minority Leader",
"speaker": {
"id": 679,
"legal_name": "Stewart Mwachiru Shadrack Madzayo",
"slug": "stewart-mwachiru-shadrack-madzayo"
},
"content": " Asante Bw. Spika. Kitu cha kwanza, nataka kukubaliana na ripoti iliyoletwa na Sen. (Prof.) Kamar kutoka Bunge la Afrika. Hili ni Bunge la muhimu sana. Nilikua mmoja wao ule muhula wa miaka mitano iliyokwisha ma nilijihusisha vilivyo. Ripoti hiyo ni ya usawa kabisa na ninaiunga mkono. Pili ni kwamba Bunge hio inaleta mataifa yote na wawakilishi wa waliochaguliwa kutoka nchi zao ili kuweza kutengeneza taratibu za jinsi Afrika inaweza fanya taratibu zake. Bunge hilo mara nyingi, tumekua tukijihusisha hususan na mambo ya kibiashara, kazi, utalii na mipaka ili kuona ya kwamba Afrika imeendelea mbele. Ni Bunge muhimu sana. Ripoti iliyokuja ni kwamba sote tuweze kuiunga mkono. Tunaiunga mkono kwa sababu inaleta Afrika karibu. Tunaweza kushirikiana ili tuone Afrika yetu inakua bora. Bw. Spika, kinachosikitisha ni kwamba unapoenda nchi za Afrika kama vile Casablanca kule Morocco inabidi utoke Afrika ili urudi nchi nyingine ndani ya Afrika. Ni jukumu mojawapo linafaa kuangaliwa. Kama waafrika ni kwa nini lazima tutoke nje ya Afrika ili tuingie nchi nyingine ndani ya Afrika? Ni kwa sababu ya uhusiano mwema tunavyoishi pamoja. Naunga mkono hii ripoti. Ni muhimu kusisitiza kwamba sisi kama waafrika tuweze kwenda nchi zote za Afrika, kuhusiana na kutembealeana."
}