GET /api/v0.1/hansard/entries/1259280/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1259280,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1259280/?format=api",
    "text_counter": 182,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Faki",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 13211,
        "legal_name": "Mohamed Faki Mwinyihaji",
        "slug": "mohamed-faki-mwinyihaji-2"
    },
    "content": "Asante Bw. Spika kwa kunipa fursa hii kuchangia Hoja ambayo imeletwa Bungeni na Sen. (Prof.) Kamar aliye mwakilishi wa Bunge hili katika Bunge la Afrika. Bunge hili linatekeleza ndoto za babu zetu na viongozi waliotangulia kama Kwame Nkrumah, Mwalimu Nyerere, hayati Kenyatta, Omar Ngwabi, Patrice Lumumba na wengineo waliokua mstari wa mbele katika miaka ya 1960s kuleta umoja wa waafrika. Ijapokuwa Bunge hilo linafanya kazi kwa sasa, bado Afrika ina hatua kubwa kupita kabla ya kua na umoja uliotarajiwa na babu zetu. Kwa mfano, safari za moja kwa moja baina ya Afrika Masharika na Kaskazini ama Magharibi. Imekua ni ndoto katika Afrika yetu. Ukiangalia safari za pamoja kutoka Mombasa na Dar-es-Salaam, mpaka sasa hakuna safari hizo. Ukiangalia Dar-es-Salaam na Mombasa ni sawa na mwendo wa Mombasa kuja Nairobi ilhali hakuna safari za ndege wala meli za moja kwa moja kati ya miji hii. Nazungumza hivi maana biashara ni mojawapo ya vitu tunaweza kutumia kuleta Afrika pamoja. Hivi sasa, bei za bidhaa hapa Kenya zimekua ghali sana. Lakini ukienda Dar-es-Salaam ama Tanga utapata kilo moja ya sukari ni Kshs120, ilhali Mombasa inauzwa Kshs240 au Kshs220. Mawasiliano yataweza kusaidia pakubwa kuleta Afrika na jamii pamoja sababu wengi waliweza kugawanywa kwa mipaka ya ukoloni iliyofanyika Berlin katika ile Berlin conference ya 1883. Tunaunga mkono uwepo wa Bunge hili la Afrika na tungependa viongozi wote wa Afrika waliunge mkono na kuhakikisha tunapata manufaa ya uongozi huu. Vile vile, tuna sheria za kikoloni hapa nchini. Kwa mfano, Maasai wa Tanzania hawezi kuja kumtembelea Sen. Olekina huko Narok. Wasomali wa Somalia hawawezi kuingia Kenya kuja kufanya biashara. Bw. Spika, Wadigo---"
}