GET /api/v0.1/hansard/entries/1259301/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1259301,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1259301/?format=api",
    "text_counter": 203,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Kinyua",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 13202,
        "legal_name": "John Kinyua Nderitu",
        "slug": "john-kinyua-nderitu-2"
    },
    "content": "Muhula uliopita sikuona hoja kama hii ya Bunge la Afrika ikiletwa katika Seneti. Hili ni jambo la kutia motisha vile Sen. (Prof.) Kamar ameleta Mswada huu. Sheria zinazotungwa kule zinafaa kuidhinishwa katika nchi zetu zote ili zitumike kwa usawa. Pesa zinazotumika katika biashara ni za aina tofauti kulingana na nchi. Kwa mfano, Kenya, Uganda na Malawi zinatumia pesa tofauti. Tunategemea Dola ya Marekani. Dola inapokosa, Afrika tunajipata katika hali mbaya. Maisha yanakuwa magumu kwa sababu kila kinaongezeka bei. Wakati Kenya ilipigania uhuru kulikuwa na watu waliojulikana kama “Mau Mau”. Sitaki kueleza kwa urefu kwa sababu inaweza kuleta hali ya sintofahamu. Sababu ya kupigania uhuru inajulikana vizuri. Nimesikiza Seneta wa Kaunti ya Siaya. Amesema vizuri kuwa kama Afrika tuna madini, kilimo, mvua na mashamba ya kutosha. Wazungu tunaowategemea hawana haja na sisi. Wanataka madini yetu. Wanataka tuwe katika hali ya vita ili watuuzie silaha kama bunduki. Naunga mkono hoja iliyoletwa ili tuziunganishe nchi zetu za Afrika kwa sababu umoja ndio nguvu. Tuweze ku---"
}