GET /api/v0.1/hansard/entries/1259541/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1259541,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1259541/?format=api",
    "text_counter": 443,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Mwaruma",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 13223,
        "legal_name": "Johnes Mwashushe Mwaruma",
        "slug": "johnes-mwashushe-mwaruma"
    },
    "content": "Wachache na ambaye pia ni Seneta wa Kitui, Sen. Wambua. Huu Mswada ulikuwa katika Seneti iliyopita, ukaenda katika Bunge la Kitaifa lakini ukaishia hapo. Bw. Spika wa Muda, ningependa kumshukuru Sen. Wambua kwa kuuleta tena Mswada huu kwa Bunge hili la kumi na tatu. Mmea wa ndengu ni mmea muhimu na vile alivyosema, huu mmea unakuzwa katika kaunti alizozitaja za Kitui, Makueni, Taita Taveta na zinginezo. Mara ya kwanza kusikia kuhusu mmea huu, nilikuwa mdogo sana. Nilikuwa kijana mdogo; mtoto mdogo na tulikuwa tunapenda kitoweo cha ndengu, haswa ikipikwa na chapati. Zamani, watoto walikuwa wanapenda sana chapati na kitoweo chetu kilikuwa ni cha ndengu kwa sababu nyama ilikuwa ghali. Kwa hivyo, kupata nyama ilikuwa si rahisi. Vile vyakula vingine ambavyo tulikuwa tunakula sana ilikuwa ugali na sukuma wiki na kabeji. Ile siku tulikuwa tunabadilisha chakula, ilikuwa siku ya kitoweo cha ndengu na chapati. Lakini mmea huu pia una umuhimu zaidi ya kuwa tu ni kitoweo. Huu ni mmea ambao unakuzwa na unahitaji mvua chache sana. Maeneo yaliyotajwa ambayo yanakuza mmea huu ni maeneo ambayo yana mvua haba kama Kaunti ya Taita Taveta, Kitui na Makueni. Ule mmea ambao unatusaidia kule ni mmea wa ndengu. Mahindi saa zingine ukiyapanda, yanafika kiwango fulani na yanakufa. Maharagwe pia kwa kiasi yanahitaji mvua nyingi. Mmea wa ndengu unahitaji mvua kidogo sana. Pia mmea huu ni kama dawa; unaleta immunity ama nguvu za kukinga mwili dhidi ya magonjwa. Mmea huu ni muhimu sana kwa sababu mahali hakuna mvua na watu hawana chakula, wanapata chakula. Lakini, mmea huu umekumbwa na changamoto si haba. Changamoto ya kwanza ni kama vile Sen. Wambua amesema; mmea huu hauna soko. Soko yake ina shida kwa sababu hakuna sera na sheria za kueelekeza kukuza na kupatia mauzo mmea huu. Wakati wa mavuno, pojo hii inakuwa nyingi sana. Na kwa sababu ya hali ya kiuchumi, wakati zao limekuwa kwa wingi, basi bei yake inateremka. Kule kwetu, wakulima wa ndengu huuza ndengu hata Kshs10 kwa kilo wakati wa mavuno na kwa sababu watu ni maskini, hawana pesa ilhali wanataka kulipia watoto wao karo, wanataka kununua sare za shule na kununulia watoto wao nguo ama kuwapeleka hospitali. Inabidi wauze kwa hiyo bei ambayo ni ndogo mno. Changamoto nyingine ni kwamba, hakuna pembejeo za kilimo wakati zinahitajika. Kwa sababu ya njaa, hawa wakulima wetu wanakula kila kitu pamoja na mbegu. Hawaachi hata mbegu kwa sababu hauwezi kuacha mbegu na una njaa. Kwa hivyo, wakati mvua inaponyesha, hawa wakulima hawana mbegu ya kupanda. Jambo lingine ni kwamba, mmea huu unapovunwa, inabidi wakulima pia wauze kwa bei ya chini kwa sababu hakuna sera na sheria ama kuwepo kwa maghala ya kuhifathi mimea hii. Kuna magunia yanayoitwa hermit bags ambayo yamebuniwa saa hizi lakini wakulima wetu, bado hawajayafikia. Hii ni mifuko spesheli ambayo inapunguza hasara baada ya mavuno. Kwa lugha ya Kimombo tunaita, post-harvest loses. Wakulima wetu hawajafikiwa na haya magunia na hizi mbinu ama madawa ya kuhifadhi ndengu hii."
}