GET /api/v0.1/hansard/entries/1259543/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1259543,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1259543/?format=api",
    "text_counter": 445,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Mwaruma",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 13223,
        "legal_name": "Johnes Mwashushe Mwaruma",
        "slug": "johnes-mwashushe-mwaruma"
    },
    "content": "Inabidi sasa kama utahifadhi kwa gunia bila kuweka dawa, ama magunia maalum, ile ndengu nyingi inaliwa na wadudu. Kwa hivyo, hasara huwa ni nyingi sana. Changamoto nyingine ni kwamba mmea huu unakua kwetu lakini wakulima wengi hawavuni kwa sababu kule kwetu ni maeneo kame; ni maeneo ambayo yamepakana na wanyama pori. Maeneo ya Kasiyau, Marungu, Kushushe, Mbololo, Bura, Mwakitau ni maeneo yote yanayokuza mmea huu wa ndengu, lakini kwa sababu wanyama pori hawajadhibitiwa kuwa mbugani, wanavuka mpaka wanakuja mahali wananchi wanaishi. Basi watu wengi pia hawavuni. Kwa hivyo, ni changamoto inayokumba huu mmea na mimea mingine kama mahindi na kadhalika kwa sababu ya changamoto hiyo. Kwa lugha ya Kimombo, tunaiita human-wildlife conflicts. Changamoto nyingine imekuwa huu mmea wa ndengu, kama mimea ingine yoyote inakumbwa na magonjwa. Na jana, tulikuwa tunajadili Mswada wa Wahudumu wa Kilimo ama Extension Officers ulioletwa na Sen. Tabitha Mutinda. Huku pia, ukosefu wa maafisa wa kilimo umekuwa ni changamoto kwa kugundua haraka magonjwa na kuangalia hitaji la huu mmea ili uwekwe dawa. Kwa hivyo, hiyo chamgamoto ya maafisa pia inafaa kuangaziwa."
}