GET /api/v0.1/hansard/entries/1259544/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1259544,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1259544/?format=api",
"text_counter": 446,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Mwaruma",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13223,
"legal_name": "Johnes Mwashushe Mwaruma",
"slug": "johnes-mwashushe-mwaruma"
},
"content": "Malengo ya huu Mswada yamekuwa ni kutoa mwelekeo ama kuweka sera na sheria zinazopeana mwelekeo wa kutekeleza ukuzaji wa huu mmea wa ndengu katika Kaunti zetu na Serikali la kitaifa, kwa sababu mimea mingi ambayo imetambulika kama mimea ya pesa ama kwa lugha ya Kimombo, cash crops, ni kama mahindi, majani chai, kahawa na kadhalika. Tayari, kuna sheria kuhusiana nazo ingawaje zimekuwa za zamani na zinahitaji marekebisho. Hatujakuwa na sheria zozote ama sera zinazotambua huu mmea kuwa mmea wa pesa ama cash crop . Kwa hivyo, huu Mswada ni muhimu na unalenga kutimiza lengo hilo. La pili pia ni kwamba, kuna uhitaji wa kuweka huu mmea ili utambulike katika soko za kimataifa, kwa sababu, ile ndengu tunayoikuza tunaikuza kwa viwango vyetu vya kaunti na Serikali ya kitaifa. Lakini je, kama ndengu yetu itakubalika katika soko za kimataifa kama uarabuni, basi inatakikana iwe ni ndengu ambayo imekuzwa kwa hali gani? Labda ni ndengu ambayo inastahili kuwekewa dawa fulani fulani, ili tukiipeleka katika soko za kimataifa, iweze kukubalika. Kwa hivyo, huu Mswada unaangazia kukuza kwa mmea huu wa ndengu kwa njia ambayo itafanya ndengu yetu ikubalike katika nchi za kimataifa. Pia katika malengo ni kwamba, huu mmea tunaukuza lakini kwa njia isiyohakikisha mazao mengi. Ili kupata mazao ya juu, tunahitaji mbegu za kisasa, zilizofanyiwa utafiti vizuri. Wataalamu wetu pia wanatakiwa kutoa mwelekezo kuhusu wakati na jinsi ya kupanda huo mmea. Haya yote ni kwa sababu Mswada huu unashinikiza kuwe na utafiti na watu wenye masomo ya kutosha, ili kuelekeza wakulima wetu."
}