GET /api/v0.1/hansard/entries/1259549/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1259549,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1259549/?format=api",
    "text_counter": 451,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Mwaruma",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 13223,
        "legal_name": "Johnes Mwashushe Mwaruma",
        "slug": "johnes-mwashushe-mwaruma"
    },
    "content": "wanapanda kwa bidii, halafu Serikali haiwasaidii kutafuta soko. Mmea huu unaharibikia manyumbani na wakati mwingine mashambani. Tukiangazia mahindi, tayari Serikali imeweka mikakati kadhaa. Ni kwa sababu ni mmea unaotambulika kama mmea wa pesa ama cash crop . Kwa mfano, wakati wakuzaji mahindi wa kaskazini mwa Bonde la Ufa wanapotoa mahindi, wakati mwingine, Serikali inanunua hayo mahindi na kuuzia wasagaji mahindi baadaye. Hii sheria inapelekea kuwe na sera kama hizo ambazo zitapelekea Serikali ya kitaifa na za kaunti kununua hii nafaka na kuhifadhi katika maghala ya kitaifa. Wakati wa njaa, tutakuwa na ndengu ya kutosha kuuzia wananchi. Tukitengeneza hii sheria, sera au kanuni, kila mkulima wa pojo apewe pesa zaidi za pembejeo na leba. Kwa Kizungu tunasema minimum guaranteed returns ."
}