GET /api/v0.1/hansard/entries/1259554/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1259554,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1259554/?format=api",
"text_counter": 456,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Mwaruma",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13223,
"legal_name": "Johnes Mwashushe Mwaruma",
"slug": "johnes-mwashushe-mwaruma"
},
"content": "La muhimu zaidi, huu Mswada unaeleza zaidi kuhusu jinsi Waziri wa Kilimo katika kaunti atahusishwa ili kuhakikisha sera na sheria zilizotungwa katika kaunti na hata ngazi ya kitaifa zimetekelezwa. Kwa mfano, huu Mswada unasema kila mkulima lazima ajisajili. Umuhimu wa kujisajili ni kwamba Serikali itajua idadi ya wakulima wa ndengu na ekari za ndengu. Kwa hivyo, wakati wa kutoa pembejeo ama mbegu, basi Serikali itaweza kufanya bajeti ili kutayarisha mbegu inayohitajika na mbolea ya ruzuku. Kumbuka changamoto moja ni kwamba hakuna mbegu wakati zinapohitajika. Pembejeo na mbolea zitakapokuja, Serikali itawasiliana na wakulima waliojisajili, kwa sababu itakuwa inajua waliko hawa wakulima na ekari zao za ndengu. Hivyo basi, watajua kila mkulima anahitaji mbegu na pembejeo kiasi fulani."
}