GET /api/v0.1/hansard/entries/1259565/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1259565,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1259565/?format=api",
"text_counter": 467,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. (Dr.) Murango",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13585,
"legal_name": "Murango James Kamau",
"slug": "murango-james-kamau"
},
"content": "Asante Bw. Spika wa Muda, kwa kunipa nafasi hii. Ushiriki wa Umma tuliofanya kuhusu ukulima katika Seneti, tulianza na Mswada ulioletwa na Sen. Wambua. Tulienda Kitui na Sen. Beth Syengo. Niliona mapenzi mengi kutoka kwa watu wa Kitui. Sen. Wambua ameleta Mswada kuhusu ndengu na Sen. Beth Syengo ameleta Mswada kuhusu pamba. Zote zinakuzwa sehemu tofauti. Tulienda mahali panaitwa Ngomeni, ambapo ni nyumbani kwa Sen. Beth Syengo. Huo wakati kulikuwa na ukame kabisa. Sababu ilioyonifanya niamue kwamba mimi nitakufa na huu Mswada kama Mwenyekiti wa Kamati ya Ukulima ni kwamba, hata kulikuwa na shida na njaa nyingi pale, wale wakulima walipata nafasi ya kutuzawadi ndengu kidogo walikuwa wamebakisha ili sisi twende nayo. Sisi tulikuwa tumeenda na magari na tulikua na chakula chetu. Niliona ukarimu mkubwa sana. Ninashukuru wakaazi wa Kitui. Ni lazima sisi Maseneta tuangalie kwa uwazi maeneo yote ya nchi ili isaidike na kile kitu wanapanda katika sehemu zile. Ukiangalia sehemu za Kitui, Voi na sehemu za juu za Pwani, wakaazi wa kule hawawezi lima kahawa, majani chai au miwa. Lakini lile zao wanaweza kusimama nalo na likawasaidia kusomesha watoto na kuwapa mahitaji ya kufanya biashara, ni zao kama ndengu, ambalo tunapanda kule Kirinyaga upande wa chini. Jambo la kushangaza ni kwamba, ndengu zilisahaulika kabisa. Bw. Spika wa Muda, naomba kusema manufaa ya ndengu katika mwili wa binadamu na virutubisho ambavyo inapea mwili wa binadamu. Utashangaa ya kwamba, ndengu ni muhimu hata kushinda nyama. Tulipokuwa tunazunguka kutoka Tseikuru, Ngomeni, Mutomo na sehemu zingine na Sen. Wambua na Sen. Beth Syengo, tuliona nyuso za wale watu waliokuwa wanatoka"
}