GET /api/v0.1/hansard/entries/1259573/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1259573,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1259573/?format=api",
"text_counter": 475,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. (Dr.) Murango",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13585,
"legal_name": "Murango James Kamau",
"slug": "murango-james-kamau"
},
"content": "inasaidia wale watu wanasumbuliwa na high blood pressure . Wale watu wanaotaka kupunguza kilo kidogo, ndengu ni mzuri sababu kuna kitu kinaitwa butylate katika ndengu. Tutakaa chini ya miti ili tuongee maneno kama haya. Lakini, cha msingi ni kwamba ndengu ni zao muhimu sana katika mwili wa binadamu. Wale wanajeshi wetu, kabla waende kupigana na Al Shabaab pande ile, wanafaa wapewe mkebe ya ndengu ili waende nayo itawasaidia. Watoto wetu shuleni wanaohangaika na utapiamlo na wale wana afya nzuri, ili kuhakikisha afya zao zinaendelea kuwa nzuri, wanafaa chakula chao kisikose ndengu, sababu tutakuwa tunazikuza hapa. Shule, idara za Serikali na hapa Seneti, tunafaa tuanze kula ndengu kama mfano bora kuonyeshana tunaunga mkono zile vitu tunafanya hapa. Tusiwe tunahubiri maji lakini tunakunywa divai. Pia kwa hoteli yetu hapa Bunge, ndengu inafaa iwekwe ili tuikule hapo ili tuweze kusaidia hawa wakulima wetu. Bw. Spika wa Muda, wakati tutasaidia wakulima wa ndengu katika kaunti zote 35, tushike miwa, majani chai, wanyama, kwa sababu ya jamii zetu za wafugaji, ukuliwa samaki na pamba tunayokuja kumalizia, tutashika Kenya nzima na hakuna mtu atasikia kama amedanganywa wakati pesa ya taifa inagawa kwenda kuimarisha mipango ya kulima na kupeana pembejeo kwa wakulima katika sehemu tofauti. Saa hii kuna mbolea ya ruzuku ambayo imeondolewa kodi na Serikali. Mkulima wa mchele na kahawa leo amepata mbolea ya ruzuku kutoka kwa Serikali. Mkulima ambaye anafaa kulima ndengu ambayo haijaorodheshwa kama mmea atapata mbolea ya kulima lini kutoka kwa Serikali?"
}