GET /api/v0.1/hansard/entries/1259709/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1259709,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1259709/?format=api",
"text_counter": 99,
"type": "speech",
"speaker_name": "Jomvu, ODM",
"speaker_title": "Hon. Bady Twalib",
"speaker": null,
"content": " Mheshimiwa Spika wa Muda, mimi ni Mjumbe wa Jomvu. Eneo Bunge la Jomvu limetengwa kutoka Eneo Bunge la Changamwe. Jomvu ilipozinduliwa 2013, nilikuwa Mbunge wa Eneo hilo. Kwa hivyo, mimi ni Mbunge wa kudumu wa Jomvu. Ninataka kuunga mkono Mswada huu na vile vile kumpongeza Mheshimiwa Ndindi Nyoro kwa kazi nzuri ambayo ameifanya. Mheshimiwa Spika wa Muda, ninachukua maneno yako uliyoyaongeea juu ya nchi ya Korea na zinginezo kwa maanani. Maneno yako ni ya ukweli kwa sababu, juzi tulizuru nchi ya Korea na tulijifunza mengi. Kwa mfano, ndani ya Seoul, kuna daraja 32 kwenye Riva. Tuliwaona kuwa watu wa maendeleo sana. Tunapoangalia yale yanayotendeka kwenye nchi zingine, inatupea matumaini na matarajio kwamba tunapopata na kuweka pesa tunayopewa, inapaswa kuwa kwenye miradi ambayo imetengewa na wala isitumike kwa ufisadi. The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor."
}