GET /api/v0.1/hansard/entries/1259710/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1259710,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1259710/?format=api",
"text_counter": 100,
"type": "speech",
"speaker_name": "Jomvu, ODM",
"speaker_title": "Hon. Bady Twalib",
"speaker": null,
"content": "Mwezi huu 30th June 2023, ndio mwisho wa kugawa pesa tulizotengewa kupitia kwa Bajeti ya Ziada ama Supplementary Budget . Na vile wenzetu walivyosema, ni vyema hizi pesa zitumike vizuri vile ilivyopangiwa kwenye Bajeti. Leo nitazungumzia Eneo la Jomvu. Kuna mahali panaitwa Jomvu Madafuni ambapo barabara ilitengenezwa chini ya Project AY09 . Hiyo barabara, inatoka Baroda na kutokea Madafuni. Pale pana kipande cha barabara takriban mita 800 pekee. Makamu wa Rais, Mhe. Gachagua alipokuja kuzindua mradi pale Bonje, alizungushwa mpaka Changamwe, kilomita tano ilhali angepitia barabara iliyokuwa takriban mita 800 kufika alipokuwa akielekea kufungua mradi. Kuna baadhi ya watu Serikalini ambao hawakutaka Makamu wa Rais aone upungufu wao. Uzuri ni kuwa niliyasema haya mbele yake. Nilimueleza kwa nini alizungushwa. Barabara ambayo angefaa apitie ilikuwa mbovu. Kwenye hiyo barabara pia, pamefanyika maandamano na watu wangu wamebaki wakilia pale siku nyingi. Ninasema haya ili pindi tu pesa zinapopatikana, zisifanyiwe ubadhirifu bali tu za miradi inayostahili. Moja ya miradi inayostahili kumaliziwa pindi tu Bajeti ya ziada itakapomalizika ni Barabara ya Jomvu-Madafuni. Ninasema haya kwa sababu huo mradi pia umetengewa pesa kutoka African Development Bank na European Union. Lakini leo hii, zimevujwa na bado baadhi ya watu wanadai malipo yao. Mwenyezi Mungu akinijalia, siku ya Jumanne, nitaleta Petition yao Bungeni kwa sababu kuna watu kule ambao waliondolewa bila kulipwa na pesa yenye iliyoko na tunahofia hii pesa itakapopatikana, itatumika kwa njia isiyofaa. Ufisadi katika nchi ya Kenya umekithiri sana. Kuna kampuni inayoitwa Synergy Gases ambayo imejadiliana na Serikali. Mwenye Kampuni akaiambia Serikali kuwa atawapunguzia milioni hamsini. Sijawaiona kampuni za kibinafsi zikisamehe Serikali ijapo hii iliyoweka hiyo mikakati na National Land Commission (NLC) na Kenya National Highway Authority(KeNHA). Mhe. Ndindi Nyoro amefanya kazi nzuri na ninaomba Serikali kuwa pesa zitakapopatikana, ziwekwe kwenye miradi. Vile vile, ninampongeza Mwenye Kiti kwa kazi nzuri. Umetuonyesha tajriba kwenye Bajeti hii ya Kenya. Asante Mhe. Spika wa Muda na Mungu aibariki hii nchi."
}