GET /api/v0.1/hansard/entries/1260381/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1260381,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1260381/?format=api",
    "text_counter": 287,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Kilifi County, ODM",
    "speaker_title": "Hon. Gertrude Mwanyanje",
    "speaker": null,
    "content": " Ahsante, Mwenyekiti wa Muda. Ninataka kuzungumzia hiki Kifungu cha kuongeza ushuru wa mafuta. Tusidanganywe. Roma haikujengwa mara moja. Serikali ya Kenya Kwanza inataka kujenga Roma wakati mmoja. Hamuwezi kuongeza ushuru wa mafuta kwa asilimia 100 - kutoka asilimia nane hadi 16. Ulisikia wapi? Mlisema Kenya haina pesa na mnataka kuongeza bei ya mafuta kwa asilimia 100. Hawa mama mboga wanaoenda sokoni wataenda na mafuta ya gari gani waweze kujikimu? Hawa bodaboda mlikuwa mnawazungumzia wataweza kufanya kazi yao vipi? Serikali msituchezee. Ushuru wa mafuta ubaki asilimia nane au urudi kwa asimilia tano, lakini sio 16. Mtajua sisi ni akina nani. Hamuwezi kufanyia Wakenya hivi. Haya siyo mliyowaambia Wakenya. Mama mboga watabeba mboga vipi na asilimia 16 ya mafuta?"
}