GET /api/v0.1/hansard/entries/1261063/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1261063,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1261063/?format=api",
"text_counter": 969,
"type": "speech",
"speaker_name": "Likoni, ODM",
"speaker_title": "Hon. Mishi Mboko",
"speaker": null,
"content": " Ahsante sana, Mhe. Mwenyekiti wa Muda. Pia mimi ninaunga mkono viongozi ambao wamekataa ushuru kwa ujenzi wa nyumba. Kwa miaka mingi, wafanyikazi wa umma hawajaongezwa mishahara. Kwanza tungefikiria tatizo hilo na kuongeza mishahara ya wafanyikazi wa umma, ndiposa tuweze kutoza ushuru katika zile pesa zao. Pesa za Wakenya zimekuwa zikitozwa ushuru tofauti mpaka mtu akipata pesa zake, anaona ni kama hakuna pesa ambayo anapata. Ikiwa mimi na mume wangu sote ni wafanyikazi wa umma na tunakatwa pesa hizo, je, tutapata nyumba mbili? Tunauliza kama tutapata nyumba moja ama mbili?"
}