GET /api/v0.1/hansard/entries/1262316/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1262316,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1262316/?format=api",
"text_counter": 401,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Madzayo",
"speaker_title": "The Senate Minority Leader",
"speaker": {
"id": 679,
"legal_name": "Stewart Mwachiru Shadrack Madzayo",
"slug": "stewart-mwachiru-shadrack-madzayo"
},
"content": "Iwapo Amerika wangefanya uchunguzi maalum, hawa magaidi wangeshikwa mapema kabla kuingia na kulipua hiyo bomu katikati mwa jiji letu la Nairobi na kuharibu majumba, kuua watu na kuwaacha wengine wakiwa vilema. Bi Spika wa Muda, tunaelewa ya kwamba kama mtu amekufa, ameumia ama amepata ulemavu wa maisha, inatakiwa apewe msaada. Wengine hulipwa malipo ya ridhaa kulingana na maumivu waliyopata. Wengine hupata majeraha ya milele, ilhali wengine wataenda hospitalini na kupona. Ukiangalia upande huo mwingine kati ya Wakenya 213, sio nambari yote; ni nambari ndogo, kwa sababu majina yalichukuliwa. Walioumia katika bomu hilo ni wengi zaidi. Wale Waamerika 12 walioumia, wote walichukuliwa na kupewa matibabu bora zaidi nchini mwao. Waamerika pia walioumia walichukuliwa kwao na kupewa malipo ya kisawasawa kulingana na accident waliopata hapa wakiwa kazini ama kujeruhiwa wakiwa ofisini mwao. Kwa nini kuwe na tofauti; Amerika iweze kulipa waamerika wao halafu Wakenya wetu wanaachwa wakiwa walala hoi ilhali wako na maumivu? Wengine walikufa na wengine mpaka leo ni walemavu. Walikatwa miguu, mikono, kupoteza macho na kuwa vipofu. Si jambo walilojipeleka wenyewe. Hapana. Ni kwa sababu ya yale yaliyotendeka pale. Walikua wametarget na nia zao ilikua wamelenga Amerika waweze kumaliza ule ubalozi, kuuwa waamerika na kufanya kila watakalo fanya kupeleka salamu Amerika. Salamu hizo zilifika Amerika kidogo, watu 12 lakini kuathiri zaidi wakenya 213. Hii si nambari ndogo. Bi. Spika wa Muda, imefika wakati sasa, zaidi ya miaka 20 ni mingi, na tunaelewa. Familia zimepoteza wapendwa wao waliokua wakifanya kazi hawakufanya tena, watoto wa kuenda shule, hawakuenda. Kuna umuhimu wa Amerika kuonyesha huruma fulani. Ndio maana jopo hili la Maseneta tisa ni jopo muhimu sana sababu litajiweka kipaumbele kuona kwamba Serikali ya Amerika imehusishwa. Rekodi za Kenyatta National Hospital zinafaa kupatikana. Hawa Maseneta tisa waweze pia kuangalia kwa kina ni nani anaweza kuchukua hili jukumu. Ikiwa ni wale Al- Shabaab ama ni kina nani, maana ilitangazwa ni wao; ikiwa ni hivyo, hili jopo lichukue nafasi hiyo kuona ya kwamba limechukua hatua ya kukaa na wizara, kuongea na waliopata majeraha, familia za waliokufa, ili waweze kupata---"
}