GET /api/v0.1/hansard/entries/1262600/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1262600,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1262600/?format=api",
"text_counter": 277,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Munyi Mundigi",
"speaker_title": "",
"speaker": null,
"content": "Bw. Spika, ninakataa mambo ya kutimuliwa kutoka kwa ofisi kwa Deputy Governor wa Siaya. Wakati wa kuomba kura, gavana na deputy wake wanatembea kila mahali katika kaunti wakifanya siasa lakini tunajua wakati wameingia ofisini, deputy governor anachukuliwa kama mtoto wa shule; mtu ambaye hana maana yoyote. Nina nina ushuhuda wya kusema haya. Pale Embu wakati wa kipindi cha kwanza, gavana Wambora alichagua madam aliyekuwa anaitwa Dorothy. Hata hivyo wakati wa kufanya kazi, alimnyanyasa kwa sababu Dorothy hakuwa na pahali popote mpaka yule mama akawa hana maana. Alikaa na yeye mpaka wakati mwingine alimnyang’anya gari. Baada ya kipindi cha miaka mitano, muhula wa pili alichukua kijana anayeitwa Dr. Kariuki. Nataka kusema kwa kutoa mfano."
}