GET /api/v0.1/hansard/entries/1262605/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1262605,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1262605/?format=api",
    "text_counter": 282,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Munyi Mundigi",
    "speaker_title": "",
    "speaker": null,
    "content": "Kaa chini. Mhula wa pili, akachukua Dr. Kariuki. Siku moja tunakumbuka aliegesha gari la naibu gavana katika kituo polisi karibu mwezi moja. Kwa hivyo, tumeona kazi ya magavana ni kuwanyanyasa vijana wetu watakaokuwa magavana miaka ijayo. Ninakataa na kusema kama Naibu Gavana angefaa kutimuliwa, Gavana ndiye angekuwa wa kwanza kujibu maswali haya ni kwa sababu tunajua Gavana ndiye mwenye kidole katika kufanya kazi yote kama vile kufuta na kuajiri watu. Deputy governor anachukuliwa kama mtu asiyekuwa na maana. Kwa hivyo mimi ninakataa Ripoti hii. Pili, tunajua ingekuwa ni mambo ya kurusha mawe, watu wengine hawangekuwa katika Seneti wakati huu. Wakati huu wako hapo wakizungumzia kutimuliwa kwa Naibu Gavana. Kwa hivyo ninapinga na kusema kuwa Deputy Governor wa Siaya arudishwe kazini. Asante."
}