GET /api/v0.1/hansard/entries/1262663/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1262663,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1262663/?format=api",
    "text_counter": 340,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. (Dr.) Murango",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 13585,
        "legal_name": "Murango James Kamau",
        "slug": "murango-james-kamau"
    },
    "content": "Bw. Spika, Kipengee cha 158 cha sheria kuhusu usimamizi wa fedha kinasema wazi kwamba afisa mhasibu mkuu katika kaunti ni gavana. Inasemekana kwamba Dkt. Oduol alinunua kiti. Hilo ni jambo ambalo Gavana wa Siaya anafaa kuulizwa wala sio naibu wake. Tusijifanye wanafiki hapa. Ningependa kumwuliza Kiongozi wa Wachache asimame ikiwa anajua bei ya kiti alichokalia. Ikiwa anajua, tutajua kuwa Naibu wa Gavana wa Kaunti ya Siaya ana makosa. Ikiwa hajui, ni makosa kumwekelea mwenzake kosa ilhali yeye hausiki katika ununuzi wa bidhaa katika Kaunti ya Siaya."
}