GET /api/v0.1/hansard/entries/1262680/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1262680,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1262680/?format=api",
    "text_counter": 357,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. (Dr.) Murango",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 13585,
        "legal_name": "Murango James Kamau",
        "slug": "murango-james-kamau"
    },
    "content": "Waswahili husema katika mahakama ya fisi, mbuzi hawezi kupata haki. Katika hili Bunge, mimi sitaki kuhesabiwe kama mmoja anayetajwa na hawa Waswahili. Nikimalizia, Waswahili wanasema kwamba, “kibebacho kikivuja, ni nafuu kwa mchukuzi”. Inaonyesha wazi kwamba kinachovuja katika Kaunti ya Siaya ni uongozi na sio wadogo amabo wameletwa hapa kutolewa kafara ili kufurahisha wachache. Bw. Spika, waheshimiwa wakilishi wadi wa Siaya, msijiruhusu kutumika vibaya. Fanyeni kazi kwa haki. Sijasema mlitumiwa, lakini ukweli ni kwamba mnatumiwa na watu wengine. Ikiwa ni hivyo, basi afadhali kujiuzulu mwajiriwe na wale wanaowatumia vibaya. Kwa hayo mengi, nakushukuru, Bw. Spika. Naomba kuketi."
}