GET /api/v0.1/hansard/entries/1262686/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1262686,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1262686/?format=api",
    "text_counter": 363,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Madzayo",
    "speaker_title": "The Senate Minority Leader",
    "speaker": {
        "id": 679,
        "legal_name": "Stewart Mwachiru Shadrack Madzayo",
        "slug": "stewart-mwachiru-shadrack-madzayo"
    },
    "content": " Hii ni Ripoti mwafaka. Hii kamati imefanya kazi yake. Hawa watu kumi na mmoja wamepata kwamba kuna hatia dhidi ya naibu gavana. Hatia sio moja, bali zimepatikana hatia mbili dhidi yake. Kosa la kwanza na la pili. Kawaida, kosa likipatikana hata moja katika Kamati kama hii na walete hapa, Seneti huwa inaunga mkono Ripoti ile na yule mtu huwa anafaa kuachishwa kazi. Bw. Spika, tunaona ya kwamba tunao umuhimu kwamba katika lile shataka la kwanza ambayo ni mambo ya kununua bidhaa na utendakazi kinyume na ile sheria inayotambuliwa ya procurement. Katika viti vyote hivi vinavyo kaliwa na wakubwa, sijasikia kiti ambacho kinachukua zaidi ya shilingi milioni moja. Kiti hicho kililetwa mbele ya Kamati kama dhibitisho. Kila mtu alikiona. Litakuwa jambo la kusitikisha sana hivi leo ikiwa tutaangalia kiti kama kile kikiwa kimegharimu milioni moja na elfu mia moja. Kama hatia kama hii imepatikana, ni jambo la kusitikisha ikiwa sisi kama Maseneta tutakubaliana ya kwamba ni haki mtu kununua kiti kwa bei hiyo na pesa zingine zimeenda kiholela. Ninakubaliana na Ripoti kuwa kiti hicho hakikugharimu pesa hizi zote. Wamesema ukweli na hatia imepatikana. Hatua ya kumfurusha mamlakani ni lazima ichukuliwe. Kosa la pili linahusu kutumia ofisi vibaya na kuwadanganya wananchi kwa kutoa habari za uwongo. Hili ni jambo la kutisha na kusikitisha zaidi. Wewe ukipewa maamlaka, tuna imani ya kwamba utaweza kuendesha mamlaka yako kisawasawa kulingana na sheria. Kama tunavyoona huyu “ Bullfighter” ana- represent watu wa Kakamega kisawasawa. Hayuko kwenye Ripoti lakini nasema ana- represent kisawasawa. Hivi leo, baadhi ya viongozi hutumia mamlaka yao kwa njia mbaya na kusambaza uongo, ikiwa kosa kama hili limepatikana. Mtu muongo anaweza kuleta shida kubwa sana ndani ya kaunti. Kuongea mambo ya uongo kunaweza kufanya watu wakapigana, wakauana na kutenda vitu ambavyo huwezi kuvitetea vikishatendeka. Hii Ripoti tuiunge mkono na tukubaliane ya kwamba, afurushwe mamlakani na atoke kwa hayo mamlaka ya kuwa Naibu wa Gavana."
}